Maneno ya Hekima

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mithali 20 - 22)
Swahili
Year: 
2015
Quarter: 
1
Lesson Number: 
8

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: “Hekima anuwai” ndivyo ambavyo mchambuzi wa Biblia anavyorejea sehemu ya somo letu juma hili. Kauli hiyo imenipa tabasamu usoni mwangu, kwa sababu usomaji wetu katika kitabu cha Mithali juma hili unaonekana kuvurugika na wa kujirudiarudia. Jambo la kujirudiarudia ni jema – walau kwangu binafsi. Huwa ninapenda mambo yajirudierudie ili yaweze kukaa akilini mwangu. Katika madarasa ninayofundisha kwenye shule ya sheria, huwa ninafundisha baadhi ya Mithali ambazo tutajifunza leo. Ingawa ninafundisha Mithali hizo, huwa ninahitaji kujikumbusha – kitendo ambacho ni faida ya hekima anuwai inayojirudiarudia! Juma lililopita nilitofautiana kimawazo na mmojawapo wa mabosi. Nilidhani kwamba alikuwa amekosea, lakini Mithali inayohusu kuepuka ghadhabu ya mfalme ilinijia akilini. Hebu tuzame kwenye Biblia na tusome kuhusu ghadhabu ya mfalme na maelekezo mengine kwa lengo la kuwa na maisha yenye mafanikio zaidi!

  1. Ghadhabu ya Mfalme
    1. Soma Mithali 20:2 na Mithali 19:12. Je, nani ambaye ni “mfalme” maishani mwako? (Watu walio na mamlaka juu yetu.)
      1. Je, ungependa kusimama karibu na simba aungurumaye? (Kitendo hicho hakifurahishi, kutosema chochote kuhusu kuogopeshwa.)
      2. Unapotafakari kuhusu “umande juu ya majani” hisia gani zinakujia akilini? (Hisia za kufurahisha. Hisia tulivu.)
      3. Je, umegundua kwamba hizi mithali zote mbili zinaanza na maneno yanayofanana, lakini zinaishia na maonyo tofauti? Mithali moja inaelezea upande chanya unaotokana na kuwa na uhusiano mzuri na mfalme, na upande mwingine unaonya juu ya nini? (Kifo.)
    2. Soma Mithali 20:3. Tafakari migongano iliyopo dhidi ya walio na mamlaka juu yako. Je, sababu gani inaweza kukufanya utake kujibizana nao? (Majivuno ya mawazo ndio sababu kubwa. Kiburi chako kinapokusababishia ujibizane na kiongozi (bosi) wako, basi “kifo” cha kazi yako kinaweza kufuatia.)
      1. Je, kuna nyakati ambapo kujibizana na bosi wako ni jambo sahihi? (Sina uhakika kama kujibizana kuna manufaa yoyote, ingawa bosi mnyenyekevu atakuwa wazi kupokea mawazo mapya. Lakini, kuna nyakati ambazo vigezo vya uaminifu, uadilifu na haki vinatutaka tupaze sauti zetu. Tunatakiwa tu kufahamu kwamba kitendo hicho kinaweza kugharimu kazi zetu (yaani, kufukuzwa kazi).)
    3. Soma Mithali 21:1. Je, njia bora ya kushughulikia kutokubaliana na bosi wako ni ipi? (Hatupaswi kugombana, badala yake tunapaswa kumwomba Mungu. Bosi ndiye msimamizi wetu wa kazi, lakini Mungu ndiye msimamizi wa bosi (mfalme). Mungu anaweza kuuelekeza moyo wa mfalme kwenye njia aichaguayo Mungu.)
    4. Soma Mithali 21:2. Tumejadili kwamba kiburi chetu kinaweza kuwa chanzo cha kutokubaliana kwetu na “mfalme.” Je, kuna tatizo gani la kukabiliana na majivuno yetu wenyewe? (Kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kuona kiburi chetu wenyewe. Tunaweza kudai kwamba mjadala unahusu uaminifu, uadilifu au haki, lakini huenda tunajidanganya tu wenyewe.)
    5. Soma Mithali 21:4. Je, kiburi chetu kinahusikaje na jinsi tunavyoangalia mambo? (Hii ni sababu nyingine kwa nini hatuwezi kuamini mawazo yetu wenyewe suala la majivuno linapohusika. Kiburi chetu ni “taa.” Tunaona mambo kupitia kwenye majivuno yetu – na matokeo yake ni upotoshaji na dhambi.)
      1. Je, tunapaswa kufanya nini ikiwa hatuwezi kujiamini sisi wenyewe (kutokana na majivuno) katika kukabiliana na walio na mamlaka juu yetu? (Soma Mithali 20:18. Tunatakiwa kuzungumza na watu wengine ambao tunaamini hekima yao.)
    6. Soma Mithali 20:8. “Kupepeta/kupembua” ni neno linalotumika katika kutenganisha ngano na majani makavu. Mfalme anawezaje “kupepeta” kwa kutumia “macho” yake? (Mfalme makini anafahamu kinachoendelea. Kwa hiyo, ikiwa mamlaka zilizopo maishani mwako ziko makini, zitatambua utakapopendekeza jambo sahihi linalotakiwa kutekelezwa, na zitatambua pale ambapo ni majivuno yako tu ndiyo kiini cha mazungumzo yako.)
      1. Je, unapaswa kufanya nini ikiwa mamlaka iliyopo maishani mwako ni ya kiovu? (Nitabadili kazi fursa inapojitokeza.)
  2. Wavivu/Magoigoi
    1. Soma Mithali 20:4. Anguko la mtu mvivu hapa ni lipi? Je, hafanyi kazi kabisa? (Hapana. Inaonekana kwamba hafanyi kazi kwa umakini. Analima kwa wakati usio sahihi.)
      1. Kwa nini anatafuta mazao wakati alilima katika kipindi kibaya? (Anatafuta kwa sababu anatarajia kupata.)
      2. Hapo kabla tulisoma kuhusu wavivu ambao ni wazembe na wenye kupenda usingizi. Lakini, hiki kinaonekana kuwa kipengele tofauti na kuwa mvivu. Tatizo la huyu “mvivu” ni lipi? (Mtu huyu mvivu hajajifunza biashara yake. Hasomi maelekezo, hayuko makini (sio msikivu), wala hajitahidi kutenda mambo yake vizuri zaidi.)
    2. Soma Mithali 22:13. Anguko la mvivu ni lipi hapa? (Anaogopa kila kitu! Anafikiria matatizo ili kutafuta visingizio vya kutokufanya kazi.)
    3. Soma Mithali 20:5. Je, umewahi kumwita mtu “mzembe” (mvivu) isivyo sahihi?
      1. Je, tahadhari gani inatolewa hapa? (Watu wana tabia nyingi, changamani (ni wagumu kufahamika). Tunatakiwa kuwaelewa kabla hatujafikia hitimisho sahihi kuwahusu.)
    4. Soma Mithali 20:6 na Mithali 20:9. Je, sisi sote ni wavivu linapokuja suala la dhambi?
    5. Soma Mithali 20:7. Kwa dhahiri, si kila mtu ni mvivu linapokuja suala la dhambi! Soma Isaya 64:6. Je, unayalinganishaje mafungu haya mawili? (Isaya 64:6 inaendana na Mithali 20:6 na Mithali 20:9. Nadhani lengo letu ni Mithali 20:7. Manufaa yake ni kwamba tutawabariki watoto wetu kutokana na tabia yetu sahihi.)
    6. Soma Mithali 20:16. Umasikini unaweza kutokana na uvivu, lakini pia unaweza kutokana na upumbavu wa mtu. Je, tatizo la kwanza linaloelezewa hapa ni lipi? (Mtu huyu anakubali kumwajibikia mgeni. Mithali inasema kwamba ikiwa wewe ni mpumbavu sana kiasi cha kufanya hivyo, basi ni sahihi kuchukua mali yako ili iwe fundisho kwako.)
      1. Angalia nusu ya pili ya Mithali 20:16. Je, “mwanamke asiye mtiifu” anaendanaje na hili somo la upumbavu? (Unapaswa pia kuchukua mali ya mtu ambaye ni mpumbavu sana kiasi cha kukubali kuwajibika kwa mwanamke ambaye mtu mpumbavu ana uhusiano naye wa kimahaba/kimapenzi.)
      2. Rafiki wangu wa zamani, ambaye hatujaonana kwa miaka mingi, hivi karibuni alianza kutumikia kifungo gerezani. Sababu moja iliyomfanya aende jela ni kwamba malaya mmoja alitishia kwenda kwa mkewe isipokuwa tu kama rafiki wangu angempa fedha malaya huyo. Rafiki wangu aliwataarifu polisi ambao walimtishia yule malaya – na kwa dhahiri hiyo ndio sababu moja kubwa iliyomfanya aende jela. Ikiwa hoja zangu ziko sahihi, inaonekana hakuna aliye na “mikono safi” katika hali kama hii. Unadhani Mithali 20:16 inapendekeza jambo gani la kujifunza? (Dhambi za ngono zinaishia kukugharimu zaidi ya hadhi yako. Zinasababishia madhara kwa namna nyingine nyingi.)
    7. Soma Mithali 21:17. Je, ni kwa njia gani nyingine tuwezayo kuwa wavivu? (Kutumia muda mwingi sana kwenye sratehe (anasa).)
      1. Je, kupumzika si jambo jema? (Hapana. Mungu asingeamuru pumziko (Marko 2:27) endapo lisingekuwa jambo jema. Tatizo lililopo ni “kupenda” starehe – kuendekeza starehe kupita kiasi.)
    8. Soma Mithali 22:1. Rafiki wangu amepoteza jina lake jema, na kuwa mvivu ndio njia inayojielekeza kwenye jina baya. Kwa nini jina jema ni bora kuliko mali nyingi? (Lengo la utajiri ni lipi? Kwa nini watu wanataka kuwa matajiri? Kwa sehemu fulani ni ili watu wawaheshimu. Watu wawasifie. Jina jema linakupatia heshima na sifa)
  3. Matokeo Sahihi
    1. Soma Mithali 22:5. Je, inamaanisha nini “kuitunza nafsi yako?” (Kuwa makini na mawazo yako na kile kinachoshawishi mawazo yako. Dhambi inaanzia akilini. Ikiwa unataka kuepuka “miiba na mitego,” angalia sana mawazo yako.)
    2. Soma Mithali 22:6. Wazazi wana wajibu gani kwenye mafanikio ya watoto wao? (Mfundishe mwanao kumpenda Mungu na hekima ya Mungu, mafunzo hayo yatakuwa na manufaa baadaye.)
    3. Soma Mithali 22:10. Mwanzoni kabisa katika kazi yangu kanisani, nilijaribu kuwatuliza washiriki waliokuwa wakilikosoa kanisa. Je, hiyo ilikuwa njia sahihi? (Kama ambavyo fungu hili linavyopendekeza, baadaye nilijifunza kuendanana na wenye kudhihihaki. Wanatakiwa kuwa kwenye kanisa tofauti.)
    4. Soma Mithali 22:29. Matokeo ya jitihada kuzidi wengine ni yapi? (Mafanikio!)
    5. Rafiki, ikiwa uko makini kwenye makabiliano yako na watu walio kwenye mamlaka, ikiwa wewe ni muadilifu kwenye kazi yako, ikiwa utatafuta ubora na uko makini kwenye mawazo yako, maisha yako yatakuwa bora! Kwa nini usijitoe kufanya hivyo leo?
  4. Juma lijalo: Maneno ya Kweli.